Kikundi cha kigaudi cha Daesh chafanya shambulizi nchini Iraq kwa bomu la kemikali katika mji wa Musol

Kikkundi cha kigaidi cha Daesh kimetumia gesi za sumu walipokuwa katika mashambuliano na majeshi ya Iraq katika sehemu ya Mahalati ya Magharibi katika mji wa Musol nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Daesh chafanya jinai zengine nchini Iraq, ambapo magaiadi wa kikundi hicho wametumia gesi ya sumu walipokuwa katika mapambano sehemu ya Mahalat ya Magharibi katika mji wa Musol.
Mwanajeshi mmoja kutoka katika majeshi ya Iraq ameyasema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo na mwandishi wa habari wa Associated Press na kusema kuwa: kikundi cha kigaidi cha Daesh chatumia kombora liliokuwa na gesi ya Kemikali katika shambulio lake sehemu ya (Al-bar) magharibi mwa Musol.
Kwa mujibu wa shirika la habri hilo ni kwamba: katika shambulo hilo la kemikali liliofanywa na magaidi hao dhidi ya majeshi ya Iraq, yamesababisha hali ya kutoweza kupumua kwa wanajeshi saba wa jeshi la serikali ya Iraq, ambapo kwa haraka zaidi walifikishwa Hospitali ya  kijeshi iliopo karibu na sehemu hiyo kwa ajili ya matibabu.
Siku kadhaa ziliopita pia zilisambazwa habari zinazoonyesha kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh kilitumia bomu la gesi ya kemikali walipokuwa wameshambulia sehemu ya makazi ya raia wa kawaida katika mji wa Musol nchini humo.
Majeshi ya Iraq toka miezi miwili iliopita yalianza mashambulizi ya kuikomboa sehemu ya Mahalati ya Magharibi ya mji wa Musol kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo majeshi hayo ya Iraq kabla ya hapo yalifanikiwa kuikomboa sehemu yote ya Mahalati ya mashariki ya mji huo kutoka mikononi mwa kikundi cha kigfgaidi cha Daesh.
Mji wa Musol ni mji wa pili kwa ukumbwa uliopo kaskazini mwa Iraq, mji huo mpaka sasa ni miaka miwili umeingia mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo kikundi hicho cha kigaidi kilitangaza mji huo kuwa ndio makao makuu ya serikali yao inayodaiwa kuwa ni ya Kiislamu.
mwisho/290