Iraq: Abubakar Baghdadiy bado yuko hai nchini Syria

Kikundi cha kijasusi cha Iraq kimetangaza kuwa Abubakar Baghdadiy, kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh bado yuko hai ambapo hivi sasa yuko nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mkuu wa shirika la kijasusi la Iraq ametangaza kuwa Abubakar Baghdadiy, Khalifa wa kikundi cha kigaidi cha Daesh bado yuko hai ambapo anaonekana katika mipaka ya Iraq na Syria.
Mkuu wa kikundi cha (Assuqur) ambaye ni mkuu wa masuala ya Usalama na kukabiliana na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika wizara ya mambo ya ndani nchini humo, ameliambia gazeti la Al-Sabah nchini Iraq nakutoa onyo kuhusu kuvamiwa Iraq kwa mara ya pili na kikundi cha kigaidi cha Daesh, kwa kushirikiana na baadhi ya watu wanaonufaika na kuwepo vikundi vya kigaidi nchini humo, ambapo wanampango wa kukirudisha kikundi cha kigaidi cha Daesh, mwana usalama huyo amesisitiza kuwa baada ya kuukomboa mji wa Musol, wataanza kukabiliana na watu hao waliokuwa dhidi ya taifa hiyo.
Aidha amesema: hayo yote ni katika hali ambayo baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaingiria kazi za vyombo vya ulinzi nchini humo, ambapo hufanya juhudi za kuzuia majeshi ya nchi hiyo kuwakamata viongozi wakubwa wa kikundi cha Kigaidi cha Daesh, watu ambao lengo lao ni kuwavunja moyo wanajeshi wa nchi hiyo, hasa kile kilichotokea katika mashambulio ya kuikomboa Musol na kusababisha kutoroka kwa mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh, huku tukipata taarifa kuwa Abubakar Baghdadiy kuwa yuko hai na sasa yuko katika mipaka ya Syria na Iraq.
mwisho/290