Wanajeshi 12 wa Saudi Arabia waangamia baada ya ndege ya kijeshi kuanguka nchini Yemen

Wanajeshi 12 wa majeshi ya serikali ya Saudi Arabia wafa baada ya ndege yao ya kijeshi kuanguka katika mkoa wa Marib nchini Yemen

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia kwa idadi kadhaa ya wanajeshi wa Saudi Arabia zimetangazwa katika vyombo vya habari mbalimbali.
Kuangamia kwa ndege hayo kumetokea siku ya Jumanne, ambapo Helikopta ya majeshi ya Saudi Arabia imeanguka katika mkoa wa Ma`rib nchini Yemen na kupelekea kuangamia wanajeshi 12 katika jeshi hilo.
Miongoni mwa wanajeshiwaliokufa, wanane ni wanajeshi wa kawaida na wanne ni katika wanajeshi ambao walikuwa na jaraja katika jeshi hilo, mpaka sasa haijafahamika sababu iliopelekea kuwanguka, huku wakibainisha kuwa uchunguzi wa kufahamu sababu ya kuanguka kwake.
Miaka hivi ya karibu mamia ya wanajeshi wa serikali ya Saudi Arabia wameangamia kufuatia mapambano baina ya majeshi hayo na majeshi ya wananchi wa Yemen katika maeneo mbalimbali nchini humo.
mwisho/290