Shirika la Usalama la Ulaya: Abubakar Al-Baghdadiy ametiwa mbaloni

Ofisi ya katibu mkuu wa shirika la usalama la jumuia ya umoja wa Ulaya imetangaza katika mtandao rasmi wa Shirika hilo kukamatwa kwa kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: ofisi ya katibu mkuu wa shirika la usalama la umoja wa Ulaya wamedai kuwa, wanaripoti kamili ya kukamatwa kwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh “Abubakar Al-Baghdadiy” kaskazini mwa Syria.
Kwa mujibu wa ripoti ya ofisi hiyo imeelezwa kuwa; kukamatwa kwa gaidi mkuu huyo, kumetoka baada ya ufuatiliaji makini wa majeshi ya kijasusi ya Syria na Urusi, ambapo walimkamata tarehe 2 mwezi huu, alipokuwa akikimbia Musol na kuingia Syria ambapo akakamatwa katika mipaka ya Syria na Iraq.
Pamoja na kukamatwa kwake, mpaka sasa hakuna maelezo yeyote yaliotangazwa kuhusu suala hilo kutoka serikali ya Syria na Urusi, huku hali inaonyesha kuwa habari hii imetangazwa baada ya kusambaa kwa taarifa ya kutoroka kwa gaidi huyo katoka mji wa Musol, ambapo ilitangazwa kuwa gaidi huyo alikimbia haliyakuwa na majaraha makubwa kufuatia mashambulio yaliokuwa yakifanywa na majeshi ya Iraq katika mji wa Musol.
Mashambulio ya kuukomboa mji wa Musol nchini Iraq kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh yalianza toka mwezi Novemba mwaka jana, ambapo majeshi ya Iraq mpaka sasa yamefanikiwa kuyakomboa maeneo yote ya mashariki ya mji huo na sasa wako katika mashambulizi ya kuikomboa sehemu ya magharibi ya mji hio, ambao kikundi cha kigaidi cha Daesh kiliufanya kuwa ndio makao makuu ya serikali ya kigaidi.
mwisho/290